Trending News>>

Wabunge wataka matokeo ya mtihani yachunguzwe

Wabunge watatu nchini Kenya wametaka wataalam wa kimataifa wafanye ukaguzi wa kina kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2017.
Aidha Wabunge hao wamemtaka Waziri wa Elimu, Fred Matiang’i ajiuzulu katika kipindi cha wiki moja, na kama hatafanya hivyo watachukua hatua ya kuwasilisha muswaada Bungeni wa kumuondoa madarakani wakati Bunge litakapoanza shughuli zake.
Wabunge hao wamesema, wamemwandikia Spika wa Bunge la Taifa, Justin Muturi, awaite ili waweze kujadili ukweli kuhusu matokeo ya mitihani hiyo wakimtuhumu Waziri wa Elimu kwa kutoa matokeo ambayo hayajafanyiwa marekebisho yoyote, jambo lililosababisha wanafunzi wengi kufeli.
Zaidi ya asilimia 80 ya wanafunzi hawakuweza kufikia alama ya C+ na juu ya hapo katika mtihani wa kidato cha nne 2017.
Alama ya C+ ndiyo kiwango cha chini kabisa kumruhusu mwanafunzi kujiunga na chuo kikuu

No comments:

Powered by Blogger.