Trending News>>

Ufahamu Moyo Kama Pampu Muhimu Ya Asili


Moyo ni ogani muhimu katika mwili wa mwanadamu inayohusika na kusukuma damu katika sehemu mbali mbali za mwili, ili kusambaza hewa safi ya Oksijeni, kuondoa hewa ya Karbonidioksid, kusambaza virutubisho vya kuulinda na kuuboresha mwili.

Wanafunzi wa darasa la tano kutoka shule ya msingi Ilboru wakishirikiana na wanafunzi wenzao wenye ulemavu wa kusikia, wanayo furaha kuwasilisha namna walivyoweza kujifunza kuhusu moyo pamoja na walimu wao. Waliweza kuufahamu moyo unavyofanya kazi, kwa kutumia moyo wa Ng’ombe. Hii ni kwa sababu binadamu na Ng’ombe wote ni wanyama na muundo wa mioyo yao inafanana.

Moyo ni ogani inayohusika na kupampu damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, Ogani hii imeundwa kwa mishipa na misuli mingi, na ina ukubwa unokaribia ule wa ngumi yako au zaidi ya hapo na umeenea zaidi upande wa kushoto wa kifua.

Moyo ni mwembamba katika sehemu ya chini ukilinganisha na sehemu ya juu yake. Umbo lake linashabihiana sana na lile la kopa kwa muundo na uwiano wa ukubwa kati ya sehemu ya chini na juu. Kwa ndani umegawanyika katika sehemu kuu nne, ambapo vyumba viwili vya sehemu ya juu vinaitwa Orikali na vile viwili vya upande wa chini vinaitwa ventrikali.

Orikali ya kulia kazi yake ni kupokea damu isiyo na Oksijen kutoka sehemu zote za mwili na kisha damu hiyo husukumwa kwenye Ventrikali ya kulia ambayo nayo husukuma damu kwenye mapafu, kupitia mishipa ya Palmonary Atery(atery mapafu).Katika mapafu damu hutiwa Oksijen na kutolewa kabondayoksaid, kisha damu hiyo hutolewa katika mapafu kupitia Vena Kava.

Orikali ya kushoto hupokea damu iliyo na Oksijen kutoka kwenye mapafu, ambapo damu hiyo hupitishwa katika ventrikali ya kushoto, ambayo husukuma damu hiyo yenye Oksijen kwenye sehemu zote za mwili kupitia mshipa wa Aorta. Seli zetu za mwili hutumia Oksijen na kutoa Kabonidayoksaid kama uchafu, ambapo damu inapozunguka husambaza Oksijeni na kuchukua Karbonidayksaid.

Baada ya kupasua moyo wa Ng’ombe tulifanikiwa kuona vali nyingi zinazohusika na kuruhusu damu kutembea katika muelekeo mmoya pasina kurudi nyuma. Vali hizi zinafanya kazi kama koki ya maji ambapo ikifunguliwa maji hutoka na ikifungwa maji hayatoki na pia inazuia maji kutokurudi nyuma.

Tuliweza kuona vali za Orikali, Ventrikali na kwenye makutano ya mishipa ya Artery, Aorta na Moyo hivyo kufanya damu itiririke kwa kufuata muelekeo mmoja na kuzuia damu chafu isichanganyike na damu safi.

No comments:

Powered by Blogger.