Trump aitaka Zimbabwe kuacha kutumia Dola ya Marekani
Rais
wa Marekani, Donald Trump amesema utawala wake uko tayari kufanya kazi
na Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe lakini amesisitiza kuwa hilo
litawezekana iwapo taifa hilo litaacha kuendelea kutumia Dola ya
Marekani.
Amelitaka
kutotumia dola hiyo na badala yake lianzishe mfumo utakaohakikisha
linatumia sarafu yake ya Zimbabwe. Kwa miaka mingi Zimbabwe ilikoma
kutumia sarafu yake na kutumia ile ya Marekani hali ambayo ilikosolewa
vikali na wanauchumi.
Duru
za habari zimenukuu Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika, Don
Yamamoto akisema Zimbabwe anapaswa kudhibiti uchumi wake na siyo
kuendelea kutegemea sarafu ya nje.
“
Hivi leo hali ya uchumi wa Zimbabwe ni mbaya. Taifa hili linaagiza
chakula kutoka nje, taasisi zake za kiuchumi hazipo katika hali nzuri.
Wamelazimika kutumia Dola ya Marekani. Hawapaswi kutegemea sarafu ya
Marekani au taifa lingine lolote la kigeni. Haya ndiyo mageuzi
tunayopenda kuona yakifanyika sasa,” amenukuliwa waziri huyo akisema.
Amesema
Marekani iko tayari kusaidia magaeuzi ya kiuchumi na kisiasa nchini
Zimbabwe ili kurejesha taifa hilo katika hali yake ya kawaida. Hatua
hiyo imekuja huku Rais Mnangagwa akiyataka mataifa ya magharibi
kuliondolewa vikwazo taifa lake vilivyowekwa wakati wa utawala wa
mtangulizi wake, Robert Mugabe.
No comments:
Post a Comment