Tarehe 5 nisizoweza kusahau kwa mwaka 2017, ni ipi wewe huwezi sahau?
Tarehe 5 June. Ilikuwa ni kilio na simanzi siku hii, Cheikh
Tiote alifariki akiwa na miaka 30. Binafsi nilikuwa shabiki mkubwa sana
wa Tiote wakati akiwa yuko EPL pale Newcastle na tukio baya zaidi kwa
upande wangu katika soka kwa mwaka huu.
Tarehe
8 March. Soka ni mchezo wa ajabu, PSG waliwatembelea Barca siku hii
wakiwa na mtaji wa mabao 4 kwa 0 na kila mtu akawaza Barca anaaga
Champions League. Mabao ya Lioneil Messi, Neymar, Suarez na Sergio
yaliwashangaza PSG na mchezo ukaisha kwa bao 6 kwa 1, PSG wakaaga kwa
aggregate ya 6 kwa 5.
Tarehe
26 August. Huu ulikuwa usiku wa kuelekea tarehe 27 na watu wengi
tulikesha, kila mtu alikuwa na hamu kuona ni nini Floyd Money Mayweather
anaweza kufanya mbele ya Conor McGregor na round ya 10 tu THE MONEY
TEAM walishangilia baada ya Mayweather kushinda kwa TKO.
Tarehe
12 July. Inaweza ikawa inaonekana ajabu au sijui itaonekanaje lakini
kwangu hii siku sitaisahau, nilipomuona live shujaa wangu Wayne Rooney,
huu ulikuwa ujio wa klabu ya Everton nchini Tanzania na hakika hili nalo
lipo kwenye kumbukumbu zangu mwaka huu.
Tarehe
10 October. Kila mtu alikata tamaa kumuona Lioneil Messi kombe la
dunia, lakini alichofanya siku hii aliibeba Argentina mabegani na hat
trick aliyopiga vs Ecuador iliwahakikishia Waargentina safari ya kwenda
Urusi kwenye kombe la dunia mwakani
No comments:
Post a Comment