Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI
ya Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), yenye Makao yake
Makuu jijini Dar es Salaam, imezindua kituo cha Ufundi kinachojulikana
kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike
katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Makamu Mwenyekiti wa TYPF Training Centre, Saida
Babde alisema ndoto yao ni Taasisi yao kuwa dira ya mtoto wa kike nchini
Tanzania kwa namna moja ama nyingine, huku uzinduzi huo ukihudhuliwa na
watu mbalimbali akiwamo Mbunge wa Viti Maalum Zainabu Vullu na Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania, Mheshimiwa Naseem Al Najim.
"Ndoto
yetu ni kumkomboa mtoto wa kike kwa kupitia kituo chetu ambacho
kitakuwa kinafundisha mambo mbalimbali kama charahani, kompyuta na kazi
nyingine za mikono.
"Nawaomba
Watanzania kuchangamkia fursa hii ambapo tumeanzisha ndani ya uwapo wa
Taasisi yetu ya TYPF, ambapo sote kwa pamoja tuna kiu ya kumkwamua
Mtanzania,"Alisema.
Naye
Mheshimiwa Zainabu, Mbunge wa Viti Maalum aliwashukuru TYPF kwa kuguswa
na mambo ya kijamii, hususan dhamira ya kumkwamua na kumsaidia mtoto wa
kike bila kusahau wale wanaoishi kwenye mazingira magumu.
"Niwapongeze
TYPF kwa ubunifu huu ambao kimsingi unatokana na kupenda kwenu
kujitolea kwenye mambo ya kijamii, hivyo ni wajibu wenu sasa kuhakikisha
kituo kinakuwa na maadili mema ili dhamira yenu iwe na tija," Alisema
Mheshimiwa Mbunge.
Naye
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, H. E Naseem Al Najim alisema nchi
yake itaendelea kushirikiana kwa dhati na serikali ya Tanzania pamoja na
wananchi wake, bila kusahau taasisi mbalimbali ikiwamo TYPF.
"Nawapongeza
TYPF na viongozi wenu kwa kupenda kujitolea kwenye jamii, hivyo mlango
wa ofisi yangu upo wazi katika kuwasaidia watu wenye mahitaji hususan
wanawake," Alisema Balozi huyo wa Kuwait.
TYPF
ni taasisi inayojitolea katika mambo mbalimbali, ambapo mapema mwaka
huu waliandaa tukio la uchangiaji damu wa hiari, tukio lililofanyika pia
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF, Ally Bakry akitoa historia fupi ya
uanzishwaji wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF wakati wa uzinduzi wa
kituo cha Ufundi uliofanyika kituoni hapo Upanga jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu akizungumza na wageni
waalikwa wakati wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama
TYPF Training Centre pamoja na kuomba uongozi wa taasisi hiyo kujikita
zaidi kwa wasichana walioko pembezoni mwa mkoa wa Dar Es Salaam.
Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akizungumza jambo wakati
wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training
Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo
mbalimbali ya kimaisha.
Kaimu
wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF, Saida Babde akitoa ufafanuzi wa
uendeshwaji wa kituo hicho na kazi zitakazofanyika kituoni hapo wakati
wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training
Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo
mbalimbali ya kimaisha.
Mkuu
wa taasisi isiyo Serikali ya DYCCC, Hassan Akrabi(kushoto) akimkabidhi
cheti cha heshima kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem
Al-Najem(kulia) kwa mchango waliounesha wakati wa uanzishwaji wa kituo
cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya
kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
Baadhi
ya wageni wakiwa wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa kituo cha
Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya
kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
Mbunge
wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu pamoja na Balozi wa Kuwait nchini
Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem(wa pili kulia) wakikata utepe
kuashiria uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF
Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika
mambo mbalimbali ya kimaisha. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa taasisi isiyo
Serikali ya DHE Nureiyne ya Iringa, Sheikh Said Bin Abri.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu akiwa anashona kitambaa mara baada ya kuzindua kituo hicho
Mgeni
rasmi Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu, Balozi wa Kuwait
nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem pamoja na Mkuu wa taasisi isiyo
Serikali ya DHE Nureiyne ya Iringa, Sheikh Said Bin Abri wakiwa wamekaa
kwenye viti wakitumia Tarakilishi mpakato (laptop computer) wakati wa
uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre,
Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya
kimaisha
Mkuu
wa taasisi isiyo Serikali ya DYCCC, Hassan Akrabi(katikati) akitoa
ufafanuzi kuhusu huduma zinazotegemewa kutolea kwenye kituo hicho kwa
mgeni rasmi pamoja na balozi waktai wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi
kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza
watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment