Simba yapania kurudisha heshima
Klabu ambayo imeanzishwa na mtu binafsi ruksa unaweza
kuipumzisha mwaka mzima wawe wanakuimbia nyumbani kwako, sawa. Jasho la
wananchi tumeliwekea masharti na sisi hatuko peke yetu duniani, tumeiga
mifano halisia katika nchi mbalimbali
Simba inataka kufanya kweli kwenye michuano ya Afrika baada ya
kushindwa kuliwakilisha taifa kwa misimu minne mfululizo, baada ya
ratiba kutolewa na shirikisho la soka Afrika, afisa habari wa Simba
Haji Manara amesema, wanataka kuendeleza rekodi yao katika michuano hiyo
kwa sababu kwa kipindi chote ambacho hawajashiriki mashindano ya
kimataifa nchi haikuwa na uwakilishi mzuri.
Manara amesema hakuna timu ya kubeza katika soka la sasa hususan timu
ambayo imepata uwakilishi katika mashindano ya vilabu Afrika.
“Ratiba tumeipokea na tumeona ratiba ambayo ipo sawa, wengi wanaona
kwamba Djibouti ni dhaifu lakini hivyo wanadhani ni ratiba nyepesi kwetu
lakini unapozungumzia mpira sasa hivi hakuna timu dhaifu, Djibouti
unaweza ukaona ni dhaifu kwa kuangalia FIFA ranking lakini timu ambayo
imepata uwakilishi kwenye CAF Confederation hatuwezi kuidharau hata
kidogo.”
“Tutaipa umuhimu hiyo mechi na hatuta wadharau na tunaona kama
tunaenda kucheza na timu kubwa kwa sababu sisi malengo yetu sio raundi
ya kwanza, kwa sasa tunawaangalia Djibouti baada ya hapo Mungu akijalia
tukashinda tunaangalia timu inayokuja. Lengo letu ni kufanya vizuri kwa
sababu tumepigana kuipata nafasi kwa miaka minne na unajua nchi
haikupata uwakilishi mzuri kwa kipindi chote hicho kwa hiyo tunadhani
tutaenda kuendeleza rekodi yetu nzuri ya uwakilishi bora kwenye
mashindano ya vilabu Afrika.”
“Sasa hivi tunaweka sawa masuala ya kiusajili nadhani tarehe 15 au 16
nitawaita waandishi wa habari kuelezea mipango na mikakati yetu kwa
ujumla kuelekea January mpaka mwisho wa msimu huu pamoja na mashindano
ya kimataifa.”
No comments:
Post a Comment