
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mume wake Uchebe baada ya kufunga ndoa.
BAADA ya habari kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii na mwanamuziki
Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kuandika katika ukurasa wake kwamba alilala
na mpenzi wake wa zamani, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wiki moja kabla ya
kufunga ndoa, mwanamama huyo ameibuka na kumtolea maneno makali.
Mwanamuziki Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ enzi akiwa na Shilole.
Akipiga stori na
Mikito Nusunusu, Shilole ambaye
alifunga ndoa na Uchebe wiki iliyopita alisema, Nuh ni sawa na mfa maji
asiyeisha kutapatapa hivyo anatakiwa kupambana na hali yake.
“Sitaki kumzungumzia Nuh kwa sababu mimi na mume wangu tunamuona ni
mfa maji anayetapatapa tu, namshauri tu apambane na hali yake aache
kufuatilia na kutaka kuharibu maisha ya watu,” alisema Shilole.
STORI: GLADNESS MALLYA
No comments:
Post a Comment