Ramsey Noah Azuru Kabuli la Kanumba Asema "Aliondoka Kipindi Nyota Yake ya Mafanikio Ikianza Kung'aa"
NGULI wa filamu za Nigeria, Ramsey Noah amesema japokuwa miaka mingi
imepita tangu kufariki dunia kwa aliyekuwa msanii mahiri wa filamu za
Kibongo, Steven Kanumba, bado pengo lake haliwezi kuzibika katika
ulimwengu wa tasnia ya filamu.
Akizungumza katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam alikoenda
kuzuru kaburi la marehemu Steven Kanumba leo Jumamosi, Desemba 16, 2017,
Ramsey, alisema Kanumba aliondoka kipindi ambacho nyota yake ya
mafanikio ndiyo kwanza ilikuwa imeanza kung’ara na kwamba, kila
anapomkumbuka na mambo waliyoyafanya pamoja, huwa haamini kama hatamuona
tena maishani mwake
Ramsey alizuru hapa nchini kuhudhuria Tamasha la Kutambua Fursa kwa
vijana lilioandaliwa chini ya Kampuni ya Sahara, tamasha hilo
lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), juzi Alhamisi.
Katika kuzuru kaburi hilo aliongozana na mama mzazi wa marehemu
Kanumba, Flora Mtegoa, mdogo wa marehemu, Seth Bosco, wasanii wa filamu
na mashabiki wa marehemu Kanumba.
Ramsey ndiye msanii wa kwanza mkubwa nchini Nigeria kufanya filamu na
Mtanzania ambapo walifanya Moses na Devil’s Kingdom jambo ambalo
liliunganisha Bongo Movie na Nollywood hivyo kutengeneza uhusiano imara
kati ya nchi hizi mbili katika tasnia ya filamu.
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake
na aliyekuwa mpenzi wake, muigizazi Elizabeth Michael ‘Lulu’. Mwanadada
huyo kwa sasa anatumiankifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na
ya kumuua Kanumba bila kukusudia.
No comments:
Post a Comment