Rais Magufuli Atunukiwa Tuzo ya Amani Sauzi
Johannesburg, Afrika Kusini: Rais John Magufuli
ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa
kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.
Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania
tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda
tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini
Kenya.
Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa
tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa
masilahi ya mataifa yao.
Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta
ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama
ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya
Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017
yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki
na kuibuka mshindi.
“Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa
demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno
amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya
kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela
Courage).
No comments:
Post a Comment