Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Joel Bendera
Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia na wote
walioguswa na kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr Joel Nkaya
Bendera kilichotokea jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
alipokuwa anapatiwa matibabu.
Rais ameeleza kuwa amesema marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa akiwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Naibu Waziri na Mbunge na pia kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya michezo.
“Dkt. Joel Nkaya Bendera alikuwa kiongozi shupavu, mahiri na mchapakazi, alipenda kufanya kazi kwa ushirikiano na daima alitamani kupata mafanikio makubwa katika majukumu aliyokuwa nayo, hakika tutamkumbuka” – Rais John Magufuli

No comments:
Post a Comment