
Ndugu na marafiki wa Babu Seya na Papii wakiwa wamefurika nje ya Gereza la Ukonga.
BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kutoa msamaha kwa familia ya Nguza Viking aliyekuwa amehukumiwa
na mwanaye Papii Kocha kifungo cha maisha, ndugu wa familia hiyo na
marafiki wamefurika nje ya Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na
kumshukuru Rais.

Baadhi ya marafiki wa familia ya Babu Seya wakimpongeza Mbangu.
Mtandao huu umenasa baadhi ya picha zinazoonesha tukio zima eneo hilo hadi kuachiwa wanamuziki hao maarufu
ambao tayari wameingia uraiani.

Mtoto wa Babu Seya, Mbangu Nguza (katikati) naye akiwa nje ya gereza hilo.
“Tunamshukuru Mungu, tunamshukuru sana Rais
Magufuli kwa kuwasamehe ndugu zetu. Mungu ambariki,” alisema Mbangu,
mtoto wa Babu Seya.
Babu Seya na Papii wameachiwa leo baada ya
kutumikia kifungo hicho kwa takriban miaka 13 katika Sherehe za Miaka
56 ya Uhuru zilizofanyika mkoani Dodoma hii leo
No comments:
Post a Comment