Naibu Waziri wa Afya azindua programu ya kikundi mlezi kwa wanawake wajasiliamali
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile amezindua programu ya Kikundi Mlezi yenye lengo la
kuwawezesha wanawake wajasilimali wasio katika Sekta rasmi kuleana
wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza mitaji na biashara zao.
Dkt.
Ndugulile amezindua programu hiyo wakati alipofanya ziara Wilayani
Kisarawe mkoani Pwani katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi
kujishughulisha katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Dkt.Ndugulile
amesema kuwa ili kufanikisha kufikia Tanzania ya viwanda Serikali
itaendelea kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo hasa wanawake katika
kuwawezesha kuanzisha vikundi vitakayoanzisha viwanda vidogo vidogo na
vya kati.
Ameongeza
kuwa lengo la kuzindua Programu ya Kikundi Mlezi ni inalenga
kuwawezesha wanawake wasio katika Sekta rasmi kwa kuwashirikisha
wanawake wajasilimali waliokomaa katika biashara kuwalea na kuwasaidia
wanawake wajasiliamali wanaoanza shughuli hizo.
“Niseme
programu hii itasaidia kwa asilimia kubwa kuibua wanawake ambao
hawakuwa na uwezo katika kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake
kujiunga na vikundi kukuza biashara na miradi yao na hatimaye kuanzisha
viwanda vidogo na vya kati,” alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bibi.Sihaba Nkinga amesema kuwa programu ya Kikundi Mlezi itasaidia
kuwainua wanawake na kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za
uzalishaji.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bw. Musa Gama amesema
kuwa ataendelea kushirikiana na Wizara kuhamasisha wanawake kujitokeza
na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara ambazo
zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Wizara, viongozi wa Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kisarawe na
wanawake wajasiliamali kutoka Wilaya ya Kisarawe mara baada ya kumaliza
ziara yake ya kikazi mkoani hapo.
Mmoja
wa wanawake wajasiliamali Wilayani Kisarawe Bi. Lydia Jacob ameishukuru
Serikali kwa kuzindua Mpango huo utakaowawezesha wanawake kuleana na
kusaidiana katika kuanzisha na kuinuka katika biashara ambazo
zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile amefanya ziara ya siku moja mkoani Pwani na
kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake
kujishughulisha ili kusaidia kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano
ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
No comments:
Post a Comment