Mtwara: Mwanamke Amfungia Mumewe Ndani na Kisha Kumchoma Moto
Jeshi
la Polisi Mkoani Mtwara linamsaka mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina
la Zuhura Ismail (29) kwa tuhuma za kumuua mume wake baada ya kumfungia
ndani na kisha kuichoma nyumba kwa petroli.
Taarifa
hizo zimetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Lucas Mkondya, ambapo
amesema kwamba chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi, baada ya
mwanamke huyo kugundua kuwa aliyekuwa mume wake anaishi na mke mwingine,
na kuamua kumvizia nyumbani kwake kisha kuichoma moto na kusababisha
kifo chake.
"Ni
kweli Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamsaka mwanamke mmoja
ayefahamika kwa jina la Zuhura Ismail kwa tuhuma za kuichoma nyumba
aliyokuwa anaishi mume wake na mwanamke mwingine, kutokana na wivu wa
kimapenzi baada ya Zuhura kugundua kuwa mumewe anaishi na mke mwingine,
na kuamua kwenda kuchoma nyumba hiyo moto na kuwasababishia majeraha
makubwa, ambapo mumewe alipelekwa hospitali lakini kutokana na majereha
hayo makubwa alifariki dunia, lakini mwanamke aliyekuwa nae anaendelea
vizuri", amesema Kamanda Mkondya.
Aidha
Kamanda Mkondya amesema mara baada ya tukio hilo mwanamke huyo
aliyefahamika kwa jina la Zuhura Ismail alitoroka na kwenda
kusikojulikana, na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka na pindi
atakapopatikana watatoa taarifa.
No comments:
Post a Comment