Mshahara Bilioni 1 Kumpeleka Sanchez Man City
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez.
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Alexis Sanchez amepanga kuenÂdelea kuichezea
timu hiyo na kutoondoka katika diriÂsha dogo la usajili la mwezi ujao
ili aondoke mwisho wa msimu huu akale dili nono ManÂchester City.Inaelezwa kuwa ikiwa itakuwa hivyo, Sanchez ataondoka akiwa mchezaji huru na dau la usajili atalÂipwa yeye mwenyewe pamoja na mshahara wa pauni 325,000 (Sh 969m) kwa wiki huku haki za kutumia picha zake na posho zikiwa ni pauni 75,000 (Sh 223m) kwa wiki.
Ikiwa itakuwa hivyo ambapo atakuwa akilipwa pauni 400,000 (Sh bilioni 1.1) kwa wiki ambapo ataingia katika orodÂha ya wachezaji watakaokuwa wakilipwa malipo mazuri katika soka.
Sanchez, ameshakataa ofa ya kwenda kucheza soka nchini China, hivyo Man City inaamini itampata kwa dau dogo licha ya kuwa anawaniwa pia na Paris Saint-Germain.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger aligoma kumuuza mchezaji huyo na kueleza kuwa bado anamhitaji huku akiwa tayari aondoke huru laÂkini akiwa ameshakamilisha kazi anayoitaka.
Sanchez amekataa ofa kadhaa za kubaki ArseÂnala na kikubwa anataka kuondoka ili akatwae mataji.
Katika siku za hivi karibuni, kiwango chake kimeonekana kushuka lakini hilo halijaÂwashawishi Arsenal kukubali kumuuza JanuÂari.
Upande wa pili Arsenal pia inavutana na mchezaji wake mwingine, Mesut Ozil ambaye naye hajasaini mkataba mpya huku ikielezwa kuwa anawaniwa na Manchester United na Barcelona.
No comments:
Post a Comment