Mbunge Mwingine CHADEMA Huenda akatangaza Maamuzi Magumu Leo
Mbunge
wa Chadema, Upendo Peneza amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada
ya mbunge huyo kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kueleza
atakachozungumza na wengi wameanza kutabiri huenda na yeye akatangaza
maamuzi magumu ya kukihama chama hicho.
Peneza
mbunge kutoka Mkoa wa Geita ameitisha mkutano huo kipindi ambacho
kumekuwa na vuguvugu la wabunge kukikimbia chama hicho na kujiunga na
CCM.
Mkutano
huo umeitisha ikiwa ni siku moja kupita tangu mbunge wa Siha wa
Chadema, Dk Godwin Mollel alipotangaza kuhamia CCM akiunga jitihada za
Rais John Magufuli.
No comments:
Post a Comment