Man City Yavunja Rekodi Ya Arsenal
Man City sasa imeshinda mechi 15 mfululizo na kuivuka Arsenal ambayo ilikuwa ikishikilia rekodi ya kushinda mechi 14 mfululizo lakini yenyewe ilifanya hivyo katika misimu miwili tofauti wakati City wao wamefanikisha ndani ya msimu mmoja.
Pamoja na rekodi hiyo bado City ina nafasi ya kuweka rekodi zaidi ya hapo kwa kuwa inaendelea kucheza.
Kwa takwimu hizo pia Man City imekuwa timu ya nne kwa Ulaya kushinda mechi nyingi mfululizo katika ligi kuu.
2 comments:
hahaha
Hapa lazima kieleweke maana Man City wana mwendo mbaya sana hakuna wa kuwazuia
Post a Comment