LIVE: Miili ya Wanajeshi Waliouawa DRC Yarejeshwa Nchini
Miili ya wanajeshi hao ikishushwa kwenye ndege.
MIILI ya Askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa
na waasi wakilinda amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC) imewasili nchini leo, Jumatatu, Desemba 11,2017 saa 12 jioni
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar
es Salaam.
Miili ya askari hao ikipelekwa kwenye gari ili kwenda kuhifadhiwa hospitali.
Miili ikipelekwa kwenye gari.
Wanajeshi hao waliuawa wakati wa shambulio lililotekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambapo wanajeshi wengine zaidi ya 50 walijeruhiwa.
Askari wakibeba miili ya askari wenzao.
Miili hiyo imepokelewa na Wziri wa Ulinzi na JKT, Dk Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo.
Ndege ya UN iliyokuwa imebeba miili hiyo.
Maofisa wa JWTZ waliofika kupokea miili hiyo.
No comments:
Post a Comment