Kocha Mkuu wa Timu ya Simba Joseph Omog amepewa siku 10 za mapumziko kabla ya kuanza tena majukumu ya Ukocha.
Baada ya kuwa na mapumziko ya wiki moja, juzi Jumatatu Simba ilianza mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi jijini Dar chini ya kocha msaidizi, Masoud Djuma raia wa Burundi.
Meneja wa Simba, Richard Robert, ameliambia Championi Jumatano, kuwa wanatarajia kuungana na Omog baada ya wiki moja na nusu ambazo ni zaidi ya siku kumi kwani likizo yake ni ndefu kuliko wengine.
“Vijana wanafanya mazoezi na kocha msaidizi wakati Omog akiwa mapumzikoni ambapo anatarajia kurejea kikosini baada ya wiki moja na nusu kuendelea kuwanoa vijana,” alisema Robert.
1 comment:
hahahaha
Post a Comment