Trending News>>

Iniesta: Haitapendeza Neymar Kwenda Madrid


Mshambuliaji  wa Paris Saint- Germain, Neymar.
KIUNGO mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta amesema hana hofu kuhusu Neymar kujiunga na Real Madrid lakini akakiri kuwa ikitokea hivyo haitampendeza kutokana na uhusiano wa Neymar na mastaa wengine wa Barcelona wakati alipokuwa akiichezea timu hiyo.

Iniesta amecheza na Neymar kwa miaka minne kabla ya mchezaji huyo kuondoka na kuhamia Paris Saint- Germain lakini kumekuwa na taarifa za kuwaniwa kwa ukaribu na Real Madrid.

“Chochote kinaweza kutokea kwenye soka, kuna mambo ambayo yalionekana ni vigumu kutokea na yakatokea, sitashangaa lakini haitapendeza kwa kuwa kwa kuwa ni mchezaji mzuri lakini sina hofu,” alisema Iniesta.

No comments:

Powered by Blogger.