Hatimaye Wema, Makonda ‘Bifu’ Kwisha!
Wema Sepetu na Makonda.
BAADA ya madai ya muda mrefu juu ya
uwepo wa bifu kati ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, hatimaye wikiendi iliyopita
wawili hao walikutana uso kwa uso ‘live’.Vyanzo mbalimbali vililieleza Ijumaa Wikienda kuwa, baada ya Wema kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekuwa karibu mno na viongozi wa chama hicho akiwemo mkuu huyo wa mkoa.
“Wema na Makonda sasa hivi mambo ni supa siyo dizeli. Yale yote yaliyotokea kipindi cha nyuma ilikuwa ni kama ajali kazini maana sasa hivi wapo tayari kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na kujenga nchi,” kilisema chanzo chetu.
Alicokiandika Wema kwenye Instagram yake.
Baada ya kujinea mambo mubashara, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Wema na Makonda kupitia simu zao za mkononi ili kuzungumzia hatua hiyo ambapo simu ya Wema iliita bila kupokelewa, huku ile ya Makonda ikiwa haipatikani.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Makonda aliwataja watu mbalimbali wanaodhaniwa kuhusika na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya ambapo katika listi hiyo jina la Wema lilikuwepo, jambo lililomtibua mlimbwende huyo.
STORI: Ally Katalambula, Dar | IJUMAA WIKIENDA
No comments:
Post a Comment