Trending News>>

Hatimaye magari 50 yaliyokosa mmiliki bandarini yachukuliwa

Magari 50 ya Jeshi la Polisi yaliyotelekezwa bandarini tangu mwaka 2015 yamefanikiwa kuchukuliwa na Jeshi la Polisi.

Hayo yamethibitishwa na Msemaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Janeth Ruzagi kwa kusema kuwa TPA na Jeshi la Polisi wamefikia makubaliano na kuyachukua magari hayo na tayari yameshaondolewa bandarini wiki iliyopita.

Akizungumzia magari ya polisi, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa amesema ni kweli wameyachukua magari hayo baada ya kufanya mazungumzo na TPA na mpaka sasa wameshayachukua kwa ajili ya kazi mbalimbali za polisi.

Sakata la Magari hayo liliibuliwa na Rais Dkt. John Magufuli alipotembelea Bandarini Novemba 26 mwaka huu na kukuta magari ya polisi yakiwa yamekaa kwa muda mrefu huku yakikosa mmiliki.

Rais Magufuli baada ya kubaini madudu hayo alitoa agizo la siku saba kwa Mamlaka ya Mapato( TRA), Mamlaka ya Bandari(TPA), Takukuru na Wizara ya Fedha kuhakikisha inatoa taarifa ni nani alihusika kuagiza magari 50 kupitia mgongo wa Ofisi ya Rais.

No comments:

Powered by Blogger.