
Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Ureno, Samuel Eto’o.
MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Cameroon,
Samuel Eto’o, amekanusha ripoti kwamba alikodisha ndege ya kuwarudisha
nchini Cameroon wananchi wenzake waliokuwa katika kile kilichoita utumwa
nchini Libya.

Wanaodaiwa kuwa wakimbizi nchini Libya.
Picha zikionyesha ‘watumwa’ waliokondeana waliojazwa katika chumba
kidogo na kisha baadaye kupanda ndege, zimekuwa zikionyeshwa katika
mtandao wa Malachysblog, jambo ambalo mchezaji huyo wa zamani wa klabu
ya Barceleona alikuwa kivutio kikubwa amelikanusha.

Hali ilivyo kwa ‘watumwa’ hao.

Baada ya kushuka kwenye ndege.
Posti iliyotumwa katika mtandao, inasema katika sehemu yake kwamba: “Samuel
Eto’o alitumia mamilioni ya Dola alipokodisha ndege kwa wakimbizi wote
wa Cameroon waliokuwa wamekwama Libya na walikuwa wanateswa na baadhi
yao hadi kufa.”
Eto’o amekanusha ripoti hizi katika
mtandao wa Facebook tarehe 24 Novemba na kusema hakusema atampa kila
mkimbizi Dola milioni moja. Yote haya yanatokana na wimbi la Walibya
kutaka kwenda Ulaya kwa ajii ya kutafufa maisha bora.
No comments:
Post a Comment