El Clasico: Fainali ya mwisho ya Madrid mwaka 2017, wakifungwa wasahau La Liga
Baada ya kushinda fainali ya 5 ndani mwaka 2017 dhidi ya
Gremio jumamosi iliyopita – jumamosi hii Real Madrid watacheza fainali
ya mwisho ya mwaka 2017 vs Barcelona katika ya kwanza ya msimu.
Pamoja na kwwmba huu umekuwa mwaka wa mafanikio kwa Real Madrid – wakishinda fainali 5 walizocheza mwaka 2017, huku mwaka ukiwa unaelekea ukingoni Madrid wamebakiza fainali moja.
The Clasico vs Barcelona itakayopigwa December 23 – Los Blancos wataingia kwenye mchezo huo wakiwa pointi 11 nyuma ya mahasimu wao, ingawa wana mchezo mmoja mkononi.
Ushindi wa nyumbani kwa Zinedine Zidane utawarudisha Madrid katika mbio za ubingwa, matokeo mengine yoyote ya tofauti yatakuwa yanamaanisha mlima mrefu zaidi wa kuupanda katika kutetea taji lao la La Liga.
Baada ya kushinda makombe 5 mwaka 2017 wanahitaji kushinda mchezo wa jumamosi hii ili kuweka hai ndoto za kuongeza taji la sita miezi mitano ijayo.
Kwa mara ya kwanza Zidane atakuwa na kikosi chake chote katika mchezo wa La Liga ndani ya msimu huu. Lakini wanaumana na Barcelona ambayo imeimarika na yenye rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja msimu huu kwenye La Liga – kiujumla wamecheza mechi 22 bila kupoteza katika mashindano yote.
Hata hivyo Barcelona watamkosa beki kisiki Samuel Umtiti ambaye alipata majeraha wiki 3 zilizopita. Ousmane Dembele bado hajatengamaa kwa 💯 kucheza soka, hivyo ataukosa mchezo huo, wakati Rafinha anatarajia kurudi dimbani baada ya kupona misuli ya goti.

No comments:
Post a Comment