DENTI MBUNGE UDSM, ALIYEVUJISHA PICHA ZA BWENI LENYE NYUFA, AACHIWA HURU
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa na kuachiliwa kwa dhamana, denti Dawson Kumbusho, ambaye ni mbunge wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa kosa la uzushi wa kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii na kusambaza picha za jengo la bweni la chuo hicho lenye nyufa.
Akizungumza na wanahabari leo, ofisini kwake. Kamanda Mambosasa
amesema kuwa waliamua kumkamata denti huyo kwa kosa la kusambaza picha
zile kinyume na sheria. Kama angekuwa muungwana alipaswa kuwasiliana na
wamiliki wa jengo lile. Hata hivyo, kwa sasa ameaachiwa kwa dhamana.
“Sisi kama jeshi la polisi baada ya
kusambaa kwa picha zile tulimshikilia mwanafunzi huyo kwa ajili ya
kumuhoji baada ya kupata kile tulichokuwa tunakihitaji, ameruhusiwa
kupewa dhamana na sasa yuko nje,” alisema Kamanda Mambosasa.
Na Isri Mohamed/GPL
No comments:
Post a Comment