CCM yamtolea nje Wema Sepetu.....Yasema Haina Taarifa ya Yeye Kurudi
Baada
ya Muigizaji Wema Sepetu kutangaza kurudi ndani ya Chama Cha Mapinduzi
baada ya kukihama Februari mwaka huu, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM,
Humphrey Polepole amesema kuwa chama hicho hakina taarifa yoyote ya
kurudi kwa Wema Sepetu.
Polepole
amesema CCM ina utaratibu wa mwanachama kujiunga na chama hicho na
kuongeza kwamba chama chao siyo daladala kwamba mtu anaweza kupanda na
kushuka wakati wowote apendao, na kwamba CCM ina misingi, imani na
masharti ya uanachama.
"Kupitia
utaratibu na muundo wetu wa chama kwenye shina kisha ataandikwa kwenye
orodha ya wanachama kwenye tawi ambalo yeye ni mkaazi," amesema
Polepole.
Ameongeza
kwamba habari za Muigizaji huyo kurudi ndani ya CCM yeye amepata
taarifa mitandaoni kama jinsi watu wengine walivyozipata.
Pamoja
na hayo polepole amefafanua kuwa "Ni heri abaki huko huko (Chadema) au
akaanzie kule ambako alichukulia kadi yetu, Kuijenga CCM mpya yenye
kuheshimu nidhamu ya chama siyo kazi ndogo na inataka viongozi wenye
unyenyekevu, watumishi na wanachama wavumilivu. CCM mpya itakuwa chungu
kwa baadhi yetu lakini tamu kwa wengi wetu"
No comments:
Post a Comment