Trending News>>

Aliyefananishwa na Dk.Shika atoa wimbo wa kufafanua utata “Mimi sio Dk.Shika”

Wanasema Duniani ni watu wawili wawili hii ni kwa kufanana kwa sura hali ambayo imekuwa ikimtatiza kwa kiasi kikubwa Mtanzania Philipo Mrisho a.k.a Nandenga  ambaye hivi  karibuni mitandaoni iliibuka mijadala kwa kuelezwa kuwa ni Dk.Shika enzi za alipokuwa kijana.
Hata hivyo licha ya Philipo kuibuka na kueleza kuwa hizo ni picha zake na wala si za Dk.Shika, bado mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti ya Udaku waliendelea kutumia picha hizo kwa kuzinadi kama ndiye Dk.Shika akiwa kijana.
Mapema leo Philipo ameweza kuongea na Mtandao huu wa MO BLOG na kueleza kuwa, ameamua kuingia studio ili watu wamwelewe.
“Mimi sio Dk.Shika. Mimi ni Philipo na wala sijatokea Urusi, natokea Kusini” alieleza Philipo amabye tayari ameachia wimbo wake huo mpya wa kuwaeleza ukweli jamii.
https://youtu.be/oFu0kevahWc

No comments:

Powered by Blogger.