Trilioni 7.6 kutumika kulipa mishahara…. Bajeti ijayo
November 07, 2017
Read
Serikali inatarajia kukusanya na kutumia Sh 32.4 trilioni katika bajeti ya mwaka 2018/19.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema leo wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/19 na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/19 bungeni mjini hapa.
Mpango amesema mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa zaidi ya Sh 22 trilioni sawa na asilimia 68 ya mahitaji yote.
“Washirika wa maendeleo wanatarajia kuchangia Sh 3.7 trilioni katika bajeti,”amesema Dk Mpango.
Amesema Sh 20.2 trilioni ni fedha za matumizi ya kawaida wakati maendeleo ni Sh 12.2 trilioni.
Amesema Sh 7.6 trilioni zitatumika kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wa Serikali na taasisi za umma katika mwaka huo.
Amesema vipaumbele vya serikali ni vinne vya mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka wa fedha 2018/ 19. Amesema Sh 9.7 trilioni kutumika kulipa deni la Taifa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19.
Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, kugungamanisha uchumi na maendeleo ya watu, ujenzi wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji na kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa mpango.
Dk Mpango amesema deni la Taifa limeongezeka kufikia dola 26,115.2 Juni mwaka huu ikiwa ni ongezeko la asilimia 17 ikilinganishwa na dola 22,320.76 za kimarekani Juni mwaka jana.
Dk Mpango amesema msukumo mkubwa utawekwa katika mikakati ya kuongeza mapato, kupunguza gharama na matumizi ya uendeshaji wa Serikali na kudhibiti ulimbikizaji wa madeni.
Trilioni 7.6 kutumika kulipa mishahara…. Bajeti ijayo
Reviewed by Unknown
on
November 07, 2017
Rating: 5
Tags :
Kitaifa
No comments:
Post a Comment