RC Rukwa: Mwanafunzi Akipata Mimba, Kamateni Mzazi Wake Akae Selo Hadi Amtaje Aliyempa Mimba Mwanae
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakuu wa wilaya na
wakuu wa shule Mkoani humo kumkamata na kuwaweka ndani wazazi na
mwanafunzi yeyote wa kike atakayebainika kuwa na mimba hadi hapo
watakapomtaja aliyesababisha mimba hiyo.
Amesema
kuwa kumekuwa na tabia ya kumalizana kienyeji huko majumbani na matokea
yake watuhumiwa hawafikishwi sehemu husika ili waweze uwajibishwa na
hatimae kupunguza kasi hiyo ya mimba kwa wananfunzi.
“Mwalimu
Mkuu unapogundua tu kwamba mwananfunzi ana mimba mweke pembeni ita
wazazi wake, washirikishe polisi wawachukue wawekwe ndani kwa muda wa
masaa 48, hadi hapo watakapomtaja muhusika wa mimba hiyo, ukifanya hivyo
mara kadhaa mabadiliko yatatokea,” Amesisitiza
Ametoa
agizo hilo baada ya kusomewa taarifa ya shule ya sekondari Kirando,
Wilayani Nkasi wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa maabara wa shule
hiyo pamoja na na kuongea na wanafunzi, taarifa iliyobainisha kupatikana
kwa mimba saba kwa kipindi cha Januari hadi oktoba mwaka huu na kesi
zote zipo polisi.
Halikadhalika
alitahadharisha kuwa shule yeyote atakayoitembelea katika ziara yake
hiyo ya kujitambulisha katika Halmashauri nne za mkoa huo, ihakikishe
inabainisha hatua zilizochukuliwa kwa watuhumiwa na zilipofikia na si
kueleza tu idadi ya kesi na kuwepo kwa kesi hizo polisi.
Kwa
upande wake mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kirando Erneo Mgina
amesema kuwa kati ya wanafunzi saba waliopata ujauzito wanafunzi watatu
ni wa “A – Level” na wanne ni wa “O – Level” na kueleza kuwa wengi wao
hupata mimba wakati wa likizo na huwabaini pale tu wanaporudi shule na
kuwapima.
No comments:
Post a Comment