
Penniel Mungilwa ‘Penny’
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Harusi Yetu kinachorushwa kupitia
Televisheni ya Magic Swahili, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amewaasa watu
wajifunze kupitia muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Akizungumza na Star Mix Penny alisema kuwa, haipaswi kumuhukumu Lulu
na badala yake kujifunza kwani jambo kama hilo linaweza kumpata mtu
yeyote. “Jamani hakuna sababu
ya kumsema Lulu vibaya au kumcheka ila ni kujifunza kuwa tukio kama
hilo linaweza kumpata mtu yeyote hivyo mwenzio akipatwa na jambo kama
hilo ni vyema kumuombea,” alisema Penny.
No comments:
Post a Comment