Lazaro Nyalandu amjibu Waziri wa Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
Aliyekuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amemjibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kuhusu tuhuma ambazo
amezitoa juu yake wakati akizungumza bungeni jana Novemba 13, 2017.
Nyalandu
andika katika mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa anasikitishwa na
namna Dkt. Kigwangalla anavyotumia muda mwingi kumchafua mara baada ya
yeye kutangaza kujivua uanachama wa CCM na kauli anazotoa dhidi yake ni
za uongo.
Nyalandu ameandika;
INASIKITISHA
sana kuona WAZIRI Kigwangalla akitumia MUDA wake ndani ya BUNGE leo
kunichafua, kunidhihaki, na kusema UONGO na UZUSHI dhidi yangu, ikiwa ni
NJAMA za makusudi zilizopangwa kunichafua mara baada ya mimi kukihama
Chama Cha Mapinduzi -CCM. Aidha, hatua hiyo imepangwa kwa lengo la
kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi yeyote wa CCM atakayethubutu ama
kudiriki tena kukihama Chama Cha Mapinduzi CCM katika Serikali hii ya
awali ya tano. AIDHA, Waziri Kigwangalla anatumika VIBAYA, kwa kauli za
UONGO na UZUSHI aliuanza DHIDI yangu mara tu alipoteuliwa, kwa kuanza
kutoa kauli za kejeli dhidi ya UTUMISHI wangu uliotukuka ndani ya Wizara
ya Maliasili na Utalii na wenye REKODI thabiti.
NIANZE
na UZUSHI alioutoa Waziri Kigwangalla mapema leo BUNGENI, huku moyoni
mwake akiwa anajua fika kuwa ametumwa kusema UONGO dhidi ya Waziri
Nyalandu kwa lengo la kuandaa MAZINGIRA ya kumkamata na kubwa zaidi,
kudhalilisha azma ya WATANZANIA ambao WAKO tayari kwa mabadiliko ya
UONGOZI wa nchi kupitia UPINZANI. AIDHA, propaganda za Kigwangalla
ameamua zimuhusu Waziri moja tu wa Maliasili, tangu TAIFA kupata Uhuru.
Waziri huyu ni Nyalandu, jambo linalothibitisha NJAMA na Progaganda za
kuzimisha MOTO na nguvu ya umma kupitia UPINZANI, hasa baada ya kitendo
changu Cha kukihama CCM.
1)
WAZIRI Kigwangalla amekejeli kuwa Waziri Nyalandu alitumia Fedha za
Serikali kusafiri USA na mwanadada Aunt Ezekiel. -HABARI hii ilikuwa ya
KUZUSHA na ilichunguzwa na vyombo vya dola 2014 na kuthibitika ilitungwa
na ilikuwa ya UONGO. Katika Mkutano huo wa Washington, DC, Waziri
Nyalandu alialikwa na Balozi wa Tanzania, Marekani, na alipewa RUHUSA ya
maandishi na Serikali kuhutubia Mkutano huo kwa siku Moja. Wasanii wote
Walioalikwa,
akiwepo Mwanadada Aunt Ezekiel, hawakuwa na mwaliko wa Wizara ama
Serikali, bali waandaji wa Kongamano. Na Serikali haikulipa gharama
zozote kwao.(Mthibiti Na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anaweza
kuthibitisha)
2) Waziri Kigwangalla amedanganya BUNGE kuwa Waziri Nyalandu alitumia helikopta kugombea URAIS 2015.
-Habari
hii ni ya uzushi na UONGO, na Waziri atakuwa aidha hana BUSARA ambayo
angepaswa kujiridhisha na Taarifa kabla ya kuisoma Bungeni, ama
waliomtuma wamemwambia ASOME TU hivyo hivyo. UKWELI ni kuwa, Waziri
Nyalandu, alipokuwa CCM, aligombea katika kinyang’anyiro cha URAIS
kuomba kuteuliwa ndani ya CCM, na alitumia aidha usafiri wa MAGARI au
NDEGE za kawaida kwa kulipa nauli (fixed wings pale ilipobidi), hadi
mchakato ulipoisha kama uilivyoisha.
-AIDHA,
miaka yote nikiwa Mbunge wa Singida Kaskazini, nimekuwa nikifanya
kampeni za kumalizia kwa njia ya helikopta. Inawezekana Waziri
Kigwangalla haelewi hili, lakini naomba nimjulishe TU kuwa matumizi ya
helicopta ilipobidi yalisaidia kufika baadhi ya maeneo Jimboni kwangu
wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2000, 2005, 2010, na 2015.
-AIDHA,
Mwaka 2015 nilitumia Helicopter kwa SIKU TATU za kumalizia Kampeni, na
nilikodi helikopta hiyo kwa Sh milioni tano kwa siku (Jumla, milioni 15)
-Pia
ingependeza kama hamaki za Kigwangalla zingemkumbusha kuwa Waziri
Nyalandu akiwa Wizarani ALIPATIA Serikali Helikopta mpya Moja, alileta
ndege kwa matumizi ya kupambana na Ujangili, Alishawishi Benki ya dunia,
Ujerumani na USA kuleta mamilioni ya dola za kmarekani kusaidia
mapambano hayo, na kwamba alifanikiwa Sana kutokmeza ujangili nchini.
RAIS KIKWETE alikiri hili wakati wa kuzindua Tangazo la Tanzania
(Tanzania, the soul of Africa). 3) Kigwangalla amezusha kuwa Waziri
Nyalandu alitumia vibaya madaraka yake. Amezungumzia suala la Waziri
Nyalandu kutotia sahihi TOZO mpya zilizopendekezwa na TANAPA. Jambo
ambalo Waziri Kigwangalla angepaswa kulijua kabla ya kutoa kauli isiyo
sahihi Bungeni ni kuwa SAKATA la TOZO za Tanapa lilijadiliwa BUNGENI
mbele ya Spika Mama Anne Makinda, likiwa limeletwa na Kamati ya Lembeli,
na kwa kupitia Wizara, Waziri Nyalandu alilitolea ufafanuzi na
likamalizika na GN ilitolewa.
-SAKATA
la kupandishwa ghafla kwa TOZO za mahotelini zinazojulikana kama (Fixed
Rates) lilianza kabla sijawa Waziri. Aidha, kulikuwa na kesi Mahakama
Kuu, ambako hadi kufikia mwaka 2012, uamuzi wa Mahakama uliyotolewa.
Bado Nyalandu hakuwa Waziri. Aidha, nilipoteuliwa kama Waziri,
Nikatazama SAKATA hilo ambalo lilishachukua muda mrefu sana hadi kufikia
2014, mimi nilipokuwa Waziri. Sheria inasema ”Concession Fees shall be
10% of half Board”, na kulikuwa Na GN ya Serikali kuhusu TOZO hizo,
takribani kuanzia mwaka 2002. Hukumu ya Jaji wa Mahakama Kuu ilielekeza
kuwa TOZO zozote mpya ni sharti zipate GN mpya, na sheria ya msingi
ilitaka TOZO ziwe kwa asilimia (percentage), na sio TOZO za kukisia,
(fixed rate) ambazo ndio msingi mkubwa wa kupendeleana na rushwa katika
kupanga nani alipe kiwango gani Cha kodi. Baada ya kuitolea maelezo
Bungeni (na hansardi Zipo), Bunge na Wizara tulikubaliana namna ya
kulimaliza na ndivyo ilivyofanyika na GN ilitolewa. Uamuzi wangu kama
Waziri ulizingatia matakwa ya sheria na Kanuni. Waziri Kigwangalla
hajasema ukweli na amezusha kuhusu suala hili kwa sababu anazozijua
mwenyewe.
4)
Sakata la VITALU: Inasikitisha SANA na inatia AIBU kwamba Waziri
atalihadaa BUNGE kwamba Waziri Nyalandu amehusika na kuuza VITALU au
kugawa VITALU, na baya Zaidi kwa NJIA ya RUSHWA. -Sheria ya Wanyamapori
inatamka wazi kuwa VITALU vitagawiwa kwa wawindaji kwa kila baada ya
miaka MITANO. -Mara ya mwisho VITALU vimegawiwa Januari, 2017. Nyalandu
hakuwa WAZIRI. (Waziri alikuwa Mh. Prof Maghembe)
-Kabla ya hapo, VITALU viligawiwa mwaka 2013. Nyalandu hakuwa Waziri. (Waziri alikuwa Mh Maige)
Hii ni AIBU sana na natumaini kwa Waziri Kigwangalla na wanaomtuma wangetamani sana miaka ibadilike ili isomeke Waziri Nyalandu.
5)
Waziri Kigwangalla amedai kuwa Waziri Nyalandu alikuwa anafanyia Kazi
katika Chumba maalumu katika hoteli ya Serena. Naomba Waziri
Kigwangalla, athibitishe ni Chumba namba ngapi, na wahusika wa hoteli
pia wathibitishe. Kama Waziri, nilifanya Kazi katika ofisi yangu iliyopo
Wizaranya Maliasili na Utalii. Kigwangalla pia akumbuke mimi nilikuwa
MTEULE wa Rais ambaye alikuwa na vyombo vya kumsaidia kusimamia
Mawaziri.
6)
MADAI kuwa Waziri Nyalandu ALIUZA Twiga mwaka 2011/12 ni ya AIBU,
UZUSHI na UONGO kuzidi shetani mwenyewe. Mwaka 2011/12 Nyalandu alikuwa
NAIBU WAZIRI wa VIWANDA na BIASHARA! Uongo huu ni wa aibu na ni kazi ya
Shetani Lusifa mwenyewe, na MUNGU wa mbinguni awakemee wote wanaohusika.
7)
Mbwembwe hizi na kusingiziwa kunakofanywa kwa makusudi baada ya mimi
Nyalandu kukihama CCM ni aibu kwa TAIFA na ni matumizi mabaya sana ya
MADARAKA. Aidha, ifahamike kuwa Vitisho na njama dhidi yangu na familia
yangu kunakofanywa na wote wanaohusika hakutazimisha azma ya watanzania
kutaka mabadiliko ya kweli nchini. Imeandikwa, WAONGO wote, sehemu yao
ni katika ziwa liwakalo moto kwa kiberiki. Haki huinua Taifa, na uonevu
na dhuluma ni dhambi itakayowatafuna wahusika siku zote za Maisha yao.
— —— ——
Lazaro S. Nyalandu
No comments:
Post a Comment