Korea Kaskazi Yarusha Kombora Linaloweza Kuangamiza Sehemu Yoyote Duniani
KOREA Kaskazini
imelifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu lililoruka juu zaidi
na kudumu angani kwa dakika 53 kabla ya kutua katika bahari ya Japani ambapo kwa
mujibu wa Waziri wa Ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kombora
hilo ni hatari zaidi kwa sababu liweza kutua katika kona yoyote ile ya
dunia ikiwemo Marekani na kufanya maangamizi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Korea Kusini, kombora hilo liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960 ambapo mara ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake ni mwezi Septemba.
Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la nguvu za kinyuklia mwezi huo. Korea Kaskazini imeendeleza mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa utengenezaji wa makombora licha ya vikwazo ilivyowekewa.
Baraza kuu la usalama la umoja wa
mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura ili kuzungumzia
hatua hiyo ya kombora lililorushwa jana. Rais
wa Marekani Donald Trump aliarifiwa kuhusu hatua hiyo wakati ambapo
kombora hilo bado lilikuwa angani ambapo aliishia tu kusema ”Tutalishughulikia”.
No comments:
Post a Comment