Kigwangalla Alia na Chombo cha Habari Kwa Kumchonganisha na Rais Magufuli
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla amefunguka na kukilalamikia moja ya chombo cha habari na kusema kuwa kimepanga kumchafua na kumchonganisha na Rais Magufuli na kudai anatambua kwa hatua anazochukia watu wa namna hiyo watakuwa wengi
Kigwangalla amesema kuwa chombo cha habari hicho kimemsema kuwa amepingana na Rais Magufuli kwa kuruhusu mifugo iingizwe ndani ya hifadhi zote za Taifa ikiwepo Serengeti kitu ambacho yeye hakusema hivyo.
"Najua lengo ni kunichonganisha na Mamlaka iliyoniteua. Najua watu wa aina hii watakuwa wengi sana kwa sasa sababu nimegusa maslahi ya watu wengi sana kwa maamuzi magumu niliyofanya siku za karibuni, kuanzia kwenye suala la kufuta mchakato wa vibali vya uwindaji, kupambana na majangili hadi kuanza mchakato wa kurudisha kwenye umiliki wa Serikali hoteli zote zilizokuwa za Serikali kupitia Shirika letu la Tanzania 'Tourist Corporation' kwa kushindwa kwao kuziendesha kwa tija kwenye sekta ya utalii" alisema Kigwangalla
Waziri huyo amesema kuwa kabla ya kukikuchukulia hatua chombo hicho cha habari ameamua kusema na kuweka wazi kile alichokisema na kudai endapo wasiporekebisha hiyo taarifa atachukua hatua zaidi.
"Binafsi nimekisamehe chombo hiki, lakini ili wajifunze kuwa mimi si mtu wa kuchezea waombe radhi haraka kabla sijawaburuza kwa Waziri wa Habari, Dr. Mwakyembe, nikiwa na ushahidi wangu ili achukue hatua stahiki" aliandika Kigwangalla
Kigwangalla anasema alisitisha oparesheni iliyoendeshwa kwenye eneo la Kilomita 5 nje ya mpaka wa Serengeti ndani ya Pori la Loliondo ambapo kuna mgogoro wa ardhi
"Mimi nilisitisha operesheni iliyoendeshwa kwenye eneo la km 5 nje ya mpaka wa Serengeti ndani ya Pori Tengefu la Loliondo kwenye ardhi yenye mgogoro, na ni baada ya kupokea taarifa za ukiukwaji wa Sheria za vijiji, na uwepo wa minong'ono kwamba Serikali iliendesha 'operation' hiyo Kwa kutekeleza matakwa ya muwekezaji. Jambo nililoona linaichafua Serikali na Mhe. Rais. Nilifanya hivyo sababu najua kuna Kamati ya Mhe. Waziri Mkuu inashughulikia suala la mgogoro wa pori Tengefu la Loliondo" alisisitiza Kigwangalla
No comments:
Post a Comment