Trending News>>

Kelele za Mama Akifanya Mapenzi Zasababisha Mtoto Aite Polisi





NewsImages/6319986.jpg

Mama mmoja wa nchini Marekani amejikuta akiitiwa polisi na mwanae wa kike ambaye alikerwa na kelele zake za kimahaba wakati akifanya mapenzi na mpenzi wake.
Mama mmoja mkazi wa Panama City, Florida nchini Marekani alijikuta akigongewa mlango na mapolisi walioitwa na binti yake mwenye umri wa miaka 15 ambaye alikerwa na sauti za malavidavi za mama yake.

Binti wa mama huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni, aliamua kupiga simu polisi akiwaomba wamchukue wampeleke kwenye kituo cha kulelea watoto cha kanisa.

Mtoto huyo aliwapigia simu polisi majira ya saa 10 alfajiri akisema kuwa sio kwamba mama yake anamtesa au kumtelekeza bali anahisi mama yake anamvunjia heshima kwa kumsikilizisha kelele zake za mahaba wakati akiwa kwenye malavidavi.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 35 aliwaambia polisi kuwa siku ya tukio alimualika mpenzi wake nyumbani kwake na kwakuwa chumba chake na cha binti yake vinatenganishwa na ukuta tu ndio maana alikuwa akisikia mambo yaliyokuwa yakiendelea.

Baada ya maafisa wa polisi na wa kanisa kuzungumza na binti huyo hatimaye binti huyo alikubali kubaki nyumbani kwao kwakuwa zilikuwa zimebaki siku chache kabla ya kutakiwa kurudi kwenye shule yake ya bweni.

Pamoja na kasheshe hilo, polisi walimkabidhi binti huyo kijarida chenye maelezo ya haki za msingi za kila mkaaji kwenye nyumba.

No comments:

Powered by Blogger.