Trending News>>

DJ Supreme la Rock wa Marekani Kuangusha Bonge la Shoo, Dar


DJ Supreme kwenye mashine.
MKALI wa burudani wa Kimataifa kutoka Seattle, Washington, Marekani, Dj Supreme anatarajiwa kulitikisa Jiji la Dar es Salaam wikiendi hii ambapo anatarajiwa kufanya bonge la shoo kesho Alhamisi, Novemba 30.
Supreme ambaye amefanya ziara yake iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa DJ Vasley, DJ Sma na DJ FU itafanyika kwa siku tatu katika maeneo mbalimbali na Hoteli jijini Dar-es- Salaam.
Dj Supreme ambaye kwa sasa amekusanya kazi zaidi ya 50,000 anatarajiwa kuongeza nyingine akiwa hapa Tanzania. Akizungumza na vyombo vya habari, Supreme amesema.

“Niliacha kuhesabu kazi nilizozikusanya zilipofika 50,000 lakini bado kuna kazi nyingi zinazozitaka ambazo sijazipata. Kimsingi lengo langu kubwa nikiwa katika ardhi mama ya Afrika ni kukusanya kazi zenye asili ya Afrika za Vinyl.
“Ninatafuta funk, soul, disco, boogie, high life, kazi za makundi maarufu kama Asiko, Geraldo Pino, Kelenkye, Marijata, Rob, Witch, na William Onyebor. Huenda zipo mahali fulani kwenye nyumba ya mtu zikiwa zimajaa vumbi. Kama mtu anaweza kunisaidia kuzipata kazi izo nitashukuru sana,” alisema Dj Supreme.

DJ Supreme
Event hizo za muiki zimeandaliwa na kampuni mpya ya uandaaji wa Matukio mbalimbali jijini Dar-es- salaam ya Xfinity Entertainmen ambapo ratiba ya Dj Supreme nchini itahusisha pia kutembelea maeneo ya kihistoria ya Zanzibar na kukutana na mastaa wa ndani akiwemo Dj-Ommy ambapo atajifunza utamaduni wa Kiswahili.
“Ninafuraha kuja Afrika Mashariki na Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya kusikia mengi kuhusu eneo hili. Natumai nitapata fursa ya kujifunza utamaduni wa kiswahili na mziki, kukusanya kazi za kibongo na kubadilishana uzoefu na Ma DJs wa Tanzania,” alihitimisha Dj Supreme.

No comments:

Powered by Blogger.