Trending News>>

WhatsApp Yaboreshwa…Sasa Utaweza Kufuta Ujumbe Uliotuma Kwa Mtu Bahati Mbaya Kabla Hajausoma


Kwa muda mrefu watumiaji wa mtandao maarufu wa WhatsApp moja ya jambo lililokuwa linawahuzunisha na kuwakera ni pale wanaposhindwa kufuta ujumbe waliotuma kwa mtu.
Kuna wakati unaweza kutuma ujumbe fulani kwa bahati mbaya na kugundua umefanya kosa katika kuutuma ujumbe huo lakini ukashindwa kuufuta kwa sababu tayari umeshautuma.
Lakini kwa sasa jambo hilo la kufuta ujumbe uliokwisha tumwa linawezekana. Ndio, unaweza kuufuta ujumbe uliokwisha utuma iwe kwa bahati mbaya au la.

WhatsApp kupitia watumiaji wa toleo la Beta (WhatsApp Tester) wameanza kuwezesha kutumia huduma hiyo ya kufuta ujumbe uliokwisha tumwa.
WhatsApp Beta ni toleo ambalo linamuwezesha mtumiaji wake kuwa wa kwanza kila WhatsApp wanapojaribu kitu kipya. Huwa wa kwanza kupata huduma hiyo kabla ya kuwafikia watumiaji wa kawaida wa WhatsApp.
Namna ya kufuta ujumbe uliotuma ni rahisi sana. Ni kubonyeza kwa kushikilia ule ujumbe ulioutuma na kwa juu upande wa kulia kutafungua menu itakayokuwezesha kufuta ujumbe huo.
Utaweza kufuta ujumbe ndani ya dakika tano baada ya wewe kutuma, nje ya hapo ukiufuta utakuwa umefutika kwako tuu. Na pia hii haikupi uhakika ya kwamba ujumbe utakaotuma hautasomwa na uliyemtumia, ila kama uliyemtumia atakuwa amechelewa kuingia WhatsApp ndani ya hizo dakika 5 basi upo salama.
Zoezi hilo la kufuta ujumbe unaweza kulifanya kwa mtu mmoja mmoja au kwa kundi (WhatsApp group).
Na pindi ukifanikiwa kuuufuta huo ujumbe uliouandika ni kwamba uliyemtumia atapata ujumbe unaoeleza kwamba kuna meseji imefutwa.
Kama wewe ni mtumiaji wa WhatsApp Beta na bado hujafikiwa na maboresho hayo basi muda si mrefu yatakufikia. Na kama ni mtumiaji wa kawaida wa Whatsapp basi endele kusubiri mpaka huduma hiyo itakapo kufikia.
Mwisho mwa mwaka jana WhatsApp walitoa taarifa ya kuwa na mpango wakuja na wazo la kuwezesha ufutwaji wa meseji zilizotumwa.
Maboresho haya ni kwa watumiaji wote wa iOS na Android. Je wewe unapokeaje boresho hili kwa app ya WhatsApp?
TOA MAONI YAKO

No comments:

Powered by Blogger.