WATU 140,000 WATAKIWA KUSALIMISHA KADI ZA MABASI YA MWENDOKASI
Wakati mchakato wa kumpata mzabuni atakayetengeneza kadi maalumu za abiria wa mabasi ya mwendokasi Dar es Salaam (Udart) ukiendelea, Mtendaji Mkuu wa mradi wa mabasi hayo (Dart), Ronald Lwakatare amesema kadi 60,000 ndizo zinazotumika.
Katika siku za karibuni kadi za mabadi hayo zimeadimika kiasi cha wananchi kuhoji juu ya suala hilo, lakini uongozi wa Dart ukadai kuwa linashughulikiwa kwa kusaka mzabuni akayekabidhiwa jukumu hilo.
Hata hivyo, jana, Lwakatare alisema kati ya kadi 200,000 zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumika kwenye mfumo wa mabasi hayo ni kati ya kadi 50,000 hadi 60,000 zinazoonekana kutumiwa na wananchi.
Alisema kadi ambazo zinatumika kwa sasa ni sawa na asilimia 25, huku asilimia 75 zikiwa mifukoni mwa wateja ambao miongoni mwao wamo walichukua kadi mara mbili.
Lwakatare alisema kutotumika kwa kadi hizo kumechangia kuwepo kwa misururu ya abiria kwenye vituo vya mabasi yaliyopo kwenye mfumo huo. “Kusudi ni kwamba kadi moja kwa mtu mmoja, lakini inaonekana mtu mmoja anamiliki kadi zaidi ya moja jambo ambalo si sahihi,” alieleza.
Alifafanua kwamba wakati wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi huo Serikali ilinunua kadi 200,000 kutokana na makadirio iliyoyafanya kabla ya ku hours Ago Nyanduga: Serikali inawajibika kulinda haki ya watu kuishi.
No comments:
Post a Comment