Trending News>>

Rekodi inaonesha Real Madrid haijawahi kuzifunga timu hizi ugenini


Michuano ya Champions League inaendelea tena hii leo ambapo katika Group H Tottenham Hotspur watakuwa ugenini kuwakabili APOEL Nicosia lakini mchezo mgumu unaosubiriwa kwa hamu utakuwa kati ya Borussia Dortmund watakaokuwa nyumbani kuikabili Real Madrid.

Ni mchezo mgumu sana na wa kuvutia kwani matokeo wanayopata Dortmund siku za karibuni yanaacha watu waone ni jinsi gani mabingwa watetezi Real Madrid wanaweza kupata matokeo dhidi yao, lakini Real Madrid wana rekodi mbovu katika mechi za ugenini dhidi ya baadhi ya timu.

Borussia Dortmund ni moja kati ya timu ambazo zimekuwa zikiwapa wakati mgumu sana Real Madrid. Real hawajawahi kuwafunga Dortmund katika uwanja wao wa nyumbani,michezo 6 waliyotembelea Ujerumani walipigwa mechi 3 wakapata suluhu michezo mitatu.

Ukiacha Borussia Dortmund kuna Juventus, hawa ni watu wengine ambao hawajawahi kukubali kufungwa na Madrid wakiwa nyumbani. Real Madrid katika michezo 6 waliyoenda Italia wamepigwa michezo 5 wakipata suluhu 1.

Olympiacos, Madrid jiji la Athens nchini Ugiriki limekuwa gumu sana kwa upande wao kwani pamoja na tofauti za ukubwa kati ya Olympiacos ma Madrid lakini katika mara 4 Madrid walizoenda Ugiriki wamefungwa mara 1 na kupata suluhu 3.

Athletico Madrid, ubabe wa Real Madrid kwa Athletico ni katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu na viwanja vingine nje ya Hispania lakini Real hawajawahi kumfunga Athletico katika uwanja wao wa nyumbani na mara ya mwisho tu walikula bao 2.

Manchester City, Etihad napo pamekuwa mahala ambapo sio pazuri kwa Real Madrid, michezo miwili ambayo Madrid wametembelea uwanja huo wamepata suluhu mara zote mbili wakiambulia pointi mbili katika michezo miwili.

Ac Millan, hawa nao wamekuwa kizuizi kwa Real Madrid. Michezo mitatu ambayo Real Madrid wameenda San Siro walipigwa katika mechi mbili huku wakipata suluhu katika mchezo mmoja.

No comments:

Powered by Blogger.