Trending News>>

Kama sababu ni hii basi lazima Cavanni na Neymar watatwangana

Kama sababu ni hii baasi Neymar na Cavanni watatwangana tuu

Edson Cavanni na Neymar kuna mtifuano, na sio mtifuano mdogo ni mkubwa kweli kweli. Wengi tunajua kilichotokea wakati wa mchezo kati ya PSG na Lyon wakati wawili hao waligombea mpira lakini kumbe ndani ya vyumba kuliibuka makubwa.
Inadaiwa kwamba baada ya mchezo huo kuisha Cavanni alimfuata Neymar vyumbani na kumsema, Neymar alikasirika wakataka kukunjana lakini captain wa klabu hiyo Thiago Silva alisimama kati yao na kuzima ndondi hizo.
Sababu haswa ya Cavanni na Neymar kuanza kugombana mapema hivi  ni nini? Pesa na Ubinafsi, sir Alex Ferguson hakuwa anawapenda wachezaji wa America Kusini kwani alidai wako kimaslahi zaidi, Fergie hakuwa mnafiki kwani Cavanni na Neymar wanathibitisha imani yake.
Inafahamika kwamba Neymar na Edison Cavanni wote wameahidiwa bonus ambazo watapata kama wakimaliza kama wafungaji bora wa ligi, alichoahidiwa Neymar hakijafahamika lakin Cavanni ameahidiwa €1m kama akimaliza kileleni mwa ufungaji.
Hii inawafanya hawa wawili kujaribu kutumia kila nafasi uwanjani ili kupata goli, kwani wanajua fika kwamba wakiapata goli itawasaidia mwisho wa msimu kupata kiasi cha pesa toka kwa PSG kama zawadi ya mabao mengi.
Lakini sababu nyingine kubwa inayoleta mvutano kati ya Neymar na Edison Cavanni ni presha aliyonayo Neymar baada ya kuondoka Barcelona kwani kila mtu anatamani kuona atafanya nini, na hili linamfanya kutaka kuuonesha ulimwengu nini anaweza fanya akiwa pekeyake.
Tayari watu wengi walimtabiria Neymar kwamba anaweza kuchukua Ballon D’Or kama akimkimbia Messi, tayari amemkimbia lakini anashindwa kuwa mfalme PSG kwani tayari yupo Cavanni na hii kumfanya atamani zaidi mafanikio yake binafsi kuliko ya timu
Pesa na ubinafsi ndiyo sababu kubwa ya mtifuano wa wawili hawa na kwa suala hili inaonekana wazi kwamba Cavanni na Neymar hawawezi kuiva kwenye chungu kimoja na tuendelee kusubiri masumbwi kati ya hawa wawili yanakuja.

No comments:

Powered by Blogger.