Emmanuel Okwi is on Fire, Mkude ageuka Mfalme Simba...
Okwi is on fire, Mkude ageuka Mfalme Simba
Straika Emmanuel Okwi wa Simba, ameendelea kutamba katika kinyang’anyiro cha kuwania kugombea kiatu cha dhahabu,baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa Mwadui uliomalizika uliomalizika kwa Simba kushinda 3-0 katika uwanja wa Uhuru, Dar.
Okwi aliweza kuwanyanyasa mabeki wa Mwadui alivyotaka,huku akitumia udhaifu wa wa Kipa wa Mwadui aliyekuwa akitokea mara kwa mara kwa kufunga mabao ya kuchopu ambayo yalikuwa yakimfanya kipa huyo kushindwa kufanya lolote.
Licha ya kuwanyanyasa mabeki hao, alikuwa akikutana na changamoto kwa beki Abdallah Mfuko ambaye alionekana kuhesabu hatua za Okwi vizuri na kuzuia mashambulizi kadhaa ambayo Okwi alikuwa akianzisha akitokea upande wa kushoto uliokuwa ukiachwa wazi David Luhende ambaye mara nyingi alikuwa akipanda mbele kupiga krosi na kuchelewe kushuka.
Mwadui walionekana kuwa vizuri katika upande wa katikati baada ya kuwachezesha Abdallah Seseme, Awadh Juma na Razack Khalfan ambao waliweza kuwakamata viungo wa Simba Mzamiru Yassin na James Kotei.
Omog aligundua suala hilo na kumuingiza Mwinyi Kazimoto kuchukua nafasi ya Nicholas Gyan na kisha Jonas Mkude aloyechukua nafasi ya Mzamiru na walionekana kupunguza spidi ya viungo wa Mwadui.
Mkude aliteka hisia za Mashabiki kwani kunyanyuka kwake katika benchi na kwenda kupasha,mashabiki walianza kumshangilia vilivyo na hata wakati anaingia kelele ndio zilizidi zaidi baada ya mashabiki wa Simba kumshangilia kama Mfalme anavyopita mtaani.
Licha ya kuwa hajacheza mechi tangu ya ligi kuanza, Mkude alionekana kuwa fiti na kupunguza spidi ya vijana wa Mwadui ambao waliweza kutawala katika dimba hilo la kati.
Okwi anaongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara akiwa na Magoli 6 katika michezo 2, huku Jonas Mkude huu ukiwa mchezo wake wa kwanza katika ligi.
No comments:
Post a Comment