Trending News>>

Carlo Ancelotti atimuliwa Fc Bayern huku akitabasamu


Lisemwalo lipo kama halipo laja, hicho ndicho unachoweza kusema kuhusu Carlo Ancelotti. Tetesi za kufukuzwa kwake hazikuanza jana bali zilianza Ijumaa baa ya sare kati ya Bayern na Wolfburg.
Vipigo 9 katika michezo 60 ni vingi sana kwa klabu kubwa kama Bayern klabu ambayo ina ndoto za kurudisha ufalme wake barani Ulaya unaoonekana kupotea siku za karibuni.
Kwa karne ya 21 Bayern Munich hawajawahi kupokea kipigo kikubwa katika makundi ya Champions League kama walichopokea jana, huku kipigo kutoka kwa Hoffeinman kilizidi kuwakera mabosi.
Lakini pamoja na kutimuliwa kwake Carlo Ancelotti anabaki kuwa kocha pekee kutwaa vikombe vikubwa 4 katika ligi kubwa 5 barani Ulaya, amebeba Epl,Bundesliga,Serie A na Ligue 1.
Carlo Ancelotti alikuwa na mkataba na Bayern Munich hadi mwezi June mwaka 2019 lakini mkataba wake umekatishwa kama alivyofanyiwa na Chelsea mwaka 2011.
Wakati huo huo baadhi ya vyanzo vikubwa vya habari nchini Ujerumani vimedai Ancelotti hajachukia sana kufukuzwa kwake kwani tayari ana ofa kubwa ya pesa nyingi katika ligi ya China huku pia akihusishwa na kurudi Ac Millan.
Tetesi za Ancelotti kupata deal jipya kubwa nchini China zilikuwepo kabla hata ya msimu kuanza na ndip sababu kuna habari zinadai Ancelotti alipanga kuiacha Bayern kwa muda sasa.

No comments:

Powered by Blogger.