Waziri Mkuu: Marufuku Viongozi Kufanya Biashara Ya Pembejeo Kama Hawana Mashamba
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku viongozi wa Serikali kufanya
biashara ya pembejeo na vishada kama hawana mashamba ya tumbaku.
“Kuna
baadhi ya viongozi wa Serikali hapa mkoani wamejiingiza kwenye biashara
ya vishada na uuzaji wa pembejeo. Hii ni dosari. Hatutaruhusu hili hata
kidogo,” alisema.
Waziri
Mkuu alitoa onyo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 9, 2017) wakati
akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge,
viongozi wa dini, chama na Serikali kwenye mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Isike-Mwanakiyungi, mjini Tabora.
Alisema:
“Kiongozi wa Serikali ni lazima uwe shamba na ulilime kisasa ili liwe
ni shamba darasa kwa wakulima walio jirani nawe. Usifanye biashara ya
pembejeo kana huna shamba. Nanyi viongozi wa AMCOS msikubali kuuza
vishada vya viongozi wa Serikali, tukikukamata, utaenda jela.”
Alisema
endapo viongozi wataamua kulima mashamba ya zao hilo, watalazimika
kujiunga na vyama vya msingi (AMCOS) vya kwenye maeneo yao ili waweze
kuuza kupitia huko kutokana na agizo la Serikali linalokataza makampuni
kununua tumbaku bila kupitia kwenye vyama vya msingi.
Aprili
15, mwaka huu, akiwa katika ziara ya siku moja mkoani Tabora, Waziri
Mkuu aliagiza wakulima wa kujitegemea (Indepenent Farmers) na wale wa
kwenye vikundi (Associations) wote wauzie tumbaku yao kupitia kwenye
vyama vya ushirika ili kuzuia utoroshaji wa zao hilo na wakulima wasio
na madeni kulazimika kuwalipia wenzao.
No comments:
Post a Comment