Trending News>>

Story ya kusisimua ya kinda wa Liverpool aliyefunga goli vs Hoffenheim

Usiku wa August 15, 2017 kulikuwa na mechi za kuwaniakufuzu kucheza UEFA Champions League hatua ya makundi.
Kijana Trent Alexander-Arnold alizaliwa pembezoni mwa uwanja wa mazoezi wa Liverpool (Melwood) akaweka rekodi ambayo inasisimua.
Akiwa na umri wa miaka sita, alijiunga na academy ya Liverpool kumbuka amezaliwa maeneo ya jirani na klabu hiyo. Aliyekuwa kocha wa vijana Ian Barrigan alimchukua na kumjumuisha kwenye academy.
Badae akawa nahodha wa kikosi cha Liverpool U16 hadi U18. Steven Gerrard nahodha na legendary wa Liverpool katika kitabu chake kinachoelezea maisha yake alitenga sehemu na kumuelezea huyu dogo akimtabiria kuja kuwa nyota ya baadae ya Liverpool.
Dogo huyu amecheza katika ngazi zote za timu za vijana, akiwa na miaka sita aliingia kwenye academy. Amecheza katika timu za U16, U18, amecheza level zote za timu za taifa za vijana U16 hadi U20.
Jana usiku akicheza mechi yake ya kwanza ya mashindano ya Ulaya wakati Liverpool ikicheza dhidi ya Hoffenheim alifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa free kick.
Kuna mambo mengine yanahitaji ujasiri, ilikuwa ni mechi yake ya kwanza kwenye mashindano makubwa lakini alikuwa jasiri kuuchukua mpira baada ya Sadio Mane kufanyiwa madhambi akautenga na kupiga free kick iliyojaa kambani.
Liverpool wakashinda 2-1 ugenini na sasa wanasubiri mechi ya marudiano.

No comments:

Powered by Blogger.