Trending News>>

Shule zaidi ya 100 kufungwa


Manispaa ya Ilala imeendelea na zoezi la kuzufungia shule ambazo hazijasajiliwa katika Jimbo la Ukonga Dar es Salaam, ambapo inakadiriwa kuwa jumla ya shule 125 zitafungiwa.
Waziri wa Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce.
Zoezi hilo linaloendeshwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, ambapo aamewataka wazazi wenye watoto katika shule zilizofungiwa kufika katika ofisi za manispaa hiyo kuthibitisha usajili wa shule.
Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wenye shule wanaoendesha shule kinyume cha sheria, ambapo pia amewataka kufuata hatua za kiserikali katika kuendesha shule hizo
Shule hizo zilizo fungwa ni shule za msingi na awali ambazo ziko chini ya sekta binafsi, Miongoni mwa shule zilizofungiwa ni pamoja na Mbingaa Nursery & Primary school English Medium, Montessori Nursery School & Proficience College Ilala.

No comments:

Powered by Blogger.