Safari ya Zimbabwe ni kiki!? - Mke wa Roma
Mke wa rapa Roma Mkatoliki, bibie
Nancy Mshana amedai watu wanaodhani mume wake katumia kiki ya kwenda
Zimbabwe ili wimbo wake mpya uwe gumzo wapo sahihi na hafikirii kumlaumu
mtu yeyote kwani ni uhuru wa kujieleza
Akizungumza
na mwandishi wa ukurasa huu Nancy amesema kuwa hafahamu kama mumewe
anaweza kumtumia kama kupata kiki na iwapo kama ni kweli mume
wake kafanya hivyo basi kafanikiwa kwa kiasi kikubwa atakuwa ametisha
"Watu kama wanadai hii ni
kiki ni idea nzuri sana kwani katumia njia sahihi. Pia mimi naona ni
jambo zuri kama amenichagua mimi na ameona hii ndiyo njia sahihi ya ya
kukuza muziki wake mimi ninamsapoti kwani siku zote nimekuwa nikimsapoti
katika kazi zake ambazo zinatufanya chakula kifike mezani,' alifunguka.
Akizungumzia maisha ya umaarufu Nancy
anasema bado hajaona kama yana ugumu kwani yeye hajawa mtu wa
kujichanganya sana katika makundi ya watu, kitu ambacho anamuomba Mungu
kisije kikabadilika na kumbadilishia mfumo mzima wa maisha yake.
Hata hivyo mwana mama huyo alikataa kuweka wazi ni kitu gani kilichompeleka Zimbabwe mume wake
"Safari yake ilikuwa ya
ghafla sana na hajakwenda kufanya show. Lakini mimi sipendi kuweka wazi
kwani nitaharibu 'suprise' iliyoandaliwa lakini yeye akirudi atawaambia
kila kitu, sitaki kuharibu suprise mapema" alisema
Pamoja na hayo Msanii Roma
amewashawasili nchini usiku wa kuamkia jana kutoka Zimbabwe ili kuanza
'Media tour' ya wimbo wake mpya 'Zimbabwe' uliokuwa gumzo kila kona ya
mji kutokana na mashairi yake.
No comments:
Post a Comment