Trending News>>

Mugabe aingilia kesi ya mkewe

Mtandao wa habari nchini Afrika Kusini wa Eyewitness News, unasema Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ameahirisha mipango yake ya safari ili kushugulikia kesi inayomkabili mkewe nchini Afrika Kusini.
Msichana wa umri wa miaka 20 amemlaumu mke wake Rais Mugabe, Grace kwa kumpiga kwa kifaa cha umeme wakati wa mzozo kwenye hoteli moja Jumapili jioni.
Bi Grace hakufika katika kituo cha polisi jijini Johannesburg baada ya kusema kuwa angefanya hivyo na hadi sasa hajazungumza lolote kuhusu madai hayo.
Kinyume na ripoti za awali kuwa Bi Mugabe alikuwa amerejea nchini Zimbabwe, mtandao wa Eyewitness pia unasema, Bi Mugabe bado yuko nchini Afrika Kusini.
Rais Mugabe anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 37 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, (SADC), jijini Pretoria wiki hii.

No comments:

Powered by Blogger.