Trending News>>

MTUHUMIWA SHAMBULIO LA BARCELONA AFIKISHWA MAHAKAMANI

 ‎mtuhumiwa wa shambulizi la barcelona

WATU wanne wanaoshikiliwa na polisi kwa kushukiwa kuhusika na shambulio la Barcelona, wamefikishwa mahakama kuu ya Madrid kujibu mashitaka yanayowakabili.

Pia, mtuhumiwa wa shambulizi la Barcelona, Mohamed Houl Chemlal ni miongoni mwa washukiwa na amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kufanya shambulizi lililoua watu 15 na kujeruhi wengine 100.

Jaji Fernando Andreu anatarajiwa kuwasomea mashtaka ya kujihusisha na ugaidi, uhalifu na umiliki wa silaha kinyume na sheria.

Watuhumiwa hao watabaki rumande kwa muda wote ambao uchunguzi unafanyika.

Washukiwa wengine wanane waliuawa, baadhi wakipigwa risasi na wengine wakafa katika milipuko.

Kijana mwenye umri wa miaka 22 ambaye naye alikuwa mtuhumiwa shambulio la Barcelona, anayedaiwa kuwa na asili ya Morocco, Younes Abouyaaqoub, anadaiwa kuwa ndiye dereva wa gari lililolipuka na kusababisha vifo na majeruhi hao. Kijana huyo alipigwa risasi na polisi alipokuwa akijaribu kutoroka.

 ‎ ‎mtuhumiwa wa shambulizi la barcelona

No comments:

Powered by Blogger.