Trending News>>

MKWARA WA ‘INSTA’ UTAVUNJA UKIMYA WA KIBA?

MWAKA 2007, kijana Ali Salehe Kiba alitikisa kwa mara ya kwanza nafsi za wapenzi wa muziki wa kizazi kipya. Ni mwaka huo, jamii ilimfahamu na kumuweka katika orodha ya wanamuziki wenye uwezo wa juu. Taratibu jina la Ali Salehe  likafutika. Pakachipuka jina jipya linalovuma duniani kote,  Alikiba.

Cinderela ni wimbo ambao ulimfungulia milango ambayo mpaka hii leo bado haijafungwa. Haukupita muda akaachia ‘albamu’ iliyokwenda kwa jina hilohilo la ‘Cinderela’. Hii ikauza zaidi ya nakala milioni mbili!

Baada ya hapo, ulifuata mfululizo wa nyimbo kali ambazo zilipendwa na wengi. Hii ikamfanya afanikiwe kufanya wimbo pamoja na wasanii nguli wa kimataifa. Miongoni mwao alikuwamo mkongwe Robert Kelly.

King Kiba, kama mashabiki wake wapendavyo kumuita, amekaa kimya kwa muda sasa bila kuachia wimbo. Toka Aje na wimbo wake wa Aje, Kiba hajaja tena!

MKWARA WA INSTA
Akiwa na idadi ya wafuatiliaji Milioni mbili na laki moja katika ukurasa wake wa ‘instagram’, mhenga huyu, ameanza kuchimba mkwara matata. Hali hii inatafsiriwa na wengi kuwa ni upashaji wa misuli ya kuachia kitu kipya.

Maneno kadhaa yaliyoandikwa na Alikiba yanayoashiria kuwa anawaandaa watu wake kupokea chochote ni: ‘Kipusa!’ ‘Heart Breaker!’ ‘Pasua Kichwa!’ na nyingine ambayo bado ina motomoto ni ile aliyoitoa jana: ‘Unstoppable!’

Upepo wa burudani umebadilika. Kabla ya kuachia wimbo mpya, wasanii wengi wamekuwa wakiandaa mazingira ili watu wakae tayari na kazi iweze kupokelewa vyema. Hapana shaka kwamba, mkwara wa insta utavunja ukimya wa Kiba hivi punde.

#Makoba

Jiunge kutoa 'comment'  yako...
Attachments
alikiba.jpg
alikiba.jpg (33.33 KiB)

No comments:

Powered by Blogger.