Trending News>>

Baada ya tetesi nyingi sasa binamu wa Anthony Martial ataja timu atakayochezea mchezaji huyo msimu huu

Anthony Martial ni kati ya wachezaji ambao wanapendwa sana na mashabiki wa Manchester United, hata awe katika kiwango gani lakini mashabiki wamekuwa wakimkubali sana.
Msimu uliopita alikuwa na majanga mengi tangu kuwasili kwa Jose Mourinho, Martial alipoteza jezi yake namba 9 ambayo alipewa Zlatan Ibrahimovich huku akipoteza namba katika kikosi cha United.
Martial amekuwa akisemwa na kocha Mourinho kuhusu kiwango chake na tetesi zikaibuka kwamba Mfaransa huyo anaweza kuwa karibu kuondoka katika klabu ya Manchester United.
Hadi leo Martial bado hajaondoka na juzi tu alizidi kuzikonga nyoyo za mashabiki wa United baada ya kufunga bao safi na kutoa assist akitokea benchi katika mchezo dhidi ya West Ham.
Sasa binamu wa mchezaji huyo amefichua siri kuhusu uhamisho wa Martial na kusema hakuna uwezekano wowote wa nyota huyo kuondoka Manchester United na ataendelea kukipiga hapo hapo msimu huu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema “Martial hawezi kuondoka Manchester United hata kwa mkopo” kauli ambayo imezima tetesi zote za kinda huyo wa Kifaransa kukimbia vita ya namba katika klabu hiyo.
Inaonekana Martial ameamua kubaki na kuamua kupigania nafasi yake ndani ya kikosi hicho na kwa uwezo alionao na umri wake ni wazi kwamba United bado inamhitaji na mashabiki pia wasingependa kuona akiondoka.

No comments:

Powered by Blogger.