Azam Yamaliza Ziara Uganda, Yaichapa Vipers 1-0
KIKOSI cha Azam FC ya Dar es Salaam kimerejea jijini baada ya kukamilisha kambi yake ya siku kumi nchini Uganda kwa kuichapa Vipers bao 1-0 mchezo uliofanyika Uwanja wa St. Mary’s, Kitende, Uganda.
Kocha Mkuu wa kikosi cha Azam FC, Aristica Cioaba, aliendelea na mfumo wake wa kubadilisha kikosi kwa kuwapa nafasi wachezaji wote kucheza, baada ya kuingiza kikosi kipya katika mchezo huo, tofauti na kile kilichoanza kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Onduparaka.
Bao pekee la Azam FC kwenye mchezo huo uliokuwa mkali na nguvu lilifungwa na mshambuliaji Yahya Zayd kwa njia ya mkwaju wa penaltI dakika ya 29 kufuatia winga Joseph Mahundi kuangushwa ndani ya eneo la hatari. Baada ya kuhitimisha ziara hiyo, kikosi cha Azam FC kimerejea jijini Dar es salaam tayari kumalizia maandalizi ya mwisho ya ligi itakayoanza kutimua vumbi Agosti 26 mwaka huu.
Azam FC itaanzia ugenini kwa kukipiga na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Benedict Haule, Swalehe Abdallah/Himid Mao dk 57, Hamimu Karim/Bruce Kangwa dk 68, Abdallah Kheri, David Mwantika, Salmin Hoza, Joseph Mahundi/Frank Domayo dk 60, Braison Raphael, Yahya Zayd/Joseph Kimwaga dk 46, Ramadhan Singano/Masoud Abdallah dk 46, Idd Kipagwile/Salum Abubakar dk 78.
No comments:
Post a Comment