WATANZANIA WANAOTUMIA SIMU HUDUMA ZA MITANDAONI WAONGEZEKA
IDADI YA WATANZANIA WANAOTUMIA SIMU KUFANYA HUDUMA MITANDAONI YAONGEZEKA
Na Jumia Travel Tanzania
RIPOTI ya
Utalii ya mwaka 2017 iliyozinduliwa na Jumia Travel nchini Tanzania
imebainisha kuwa idadi ya watanzania wanaotumia simu katika kufanya
huduma za hoteli kwa njia ya mtandao imeongezeka na kufikia takribani
asilimia 60.
Ripoti
hiyo iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita imebainisha kuwa mpaka
kufikia mwaka 2016 watumiaji wa intaneti walikuwa ni zaidi ya milioni 19
kutoka milioni 17 ilivyokuwa mwaka 2015.
Ongezeko
hilo limechochewa kwa kiasi kikubwa na kukua na kuenea kwa matumizi ya
intaneti nchini (takribani asilimia 40 ya watanzania wamefikiwa na
intaneti nchini kote) lakini pia maendeleo ya kasi kwenye sekta ya
mawasiliano ya simu ambapo mpaka hivi sasa watanzania zaidi ya milioni
40 wanatumia huduma za simu za mkononi.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Meneja Mkaazi wa kampuni hiyo
inayojishughulisha na hudumza za hoteli na usafiri barani Afrika, Bi.
Fatema Dharsee amesema kuwa kukua kwa sekta hiyo ni ishara nzuri kwa
maendeleo ya huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao.
“Hakuna
anayeweza kubisha kwamba dunia yote kwa sasa imehamia mtandaoni kwani
ndiko kwenye urahisi na unafuu mkubwa. Inatia hamasa kuona kuwa
watanzania nao hawako nyuma katika kuyapokea na kuendana na mabadiliko
hayo. Hivi sasa karibu kila mtanzania ana simu ya mkononi tena ya kisasa
ambayo ina uwezo wa kutumia intaneti. Lakini cha kuvutia zaidi ni
kwamba kwa namna gani watu wanavyoutumia mtandao huu kwa manufaa yao
zaidi badala ya kufanya mambo hayana tija kwao,” alisema Bi. Dharsee.
“Jumia
Travel katika ripoti yetu tuliyoiwasilisha inaonyesha kwamba watanzania
wanautumia vizuri mtandao wa intaneti kupitia simu zao za mkononi kwenye
kufanya huduma zetu. Hii inamaanisha kwamba wameweza kugundua faida
zinazotokana na wao kufanya hivyo badala ya kwenda moja kwa moja
mahotelini kuulizia huduma. Kupitia mtandao wetu mteja anaweza kujionea
huduma za mahoteli zaidi ya 1000 ndani ya wakati mfupi na kuchagulia ile
inayomfaa sehemu yoyote ya Tanzania. Kwa kuongezea, ripoti yetu
imebainisha kuwa miongoni mwa huduma zinazouliziwa sana na wateja pindi
wanapoulizia hoteli ya kwenda ni upatikanaji wa mtandao wa intaneti.
Hivyo basi hii ni fursa kubwa kwa watoa huduma kuhakikisha kuwa huduma
hii inapatikana kwa uhakika na kuboreshwa zaidi,” alimalizia Bi.
Dharsee.
Hii ni
mara ya pili kwa Jumia Travel kuwasilisha Ripoti ya Utalii nchini
Tanzania ambapo mwaka 2016 walifanya hivyo pia. Miongoni mwa mambo
yaliwekwa wazi na ripoti hiyo ni kuendelea kwa kufanya vizuri kwa sekta
hiyo kwani mapato yake yameongozeka kutoka Dola za Kimarekani bilioni
1.9 mwaka 2015 na kufikia 2.1 mwaka 2016. Kiasi hiko kimechangia Dola za
Kimarekani bilioni 4.6 mwaka 2016 kutokea 4.2 za mwaka 2015 katika pato
la taifa.
Kwa
upande wa ajira, katika mwaka 2016 sekta hiyo imeajiri watanzania zaidi
ya milioni 1.3 (asilimia 11.6). Idadi hiyo inatarajiwa kukua kwa
asilimia 4.6 ndani yam waka huu wa 2017 na kufikia zaidi ya milioni 1.4.
Hivyo kuifanya mojawapo ya sekta muhimu katika uchangiaji wa uchumi na
pato la taifa kwa ujumla.
Mbali
na kuwasilisha ripoti hiyo, Jumia iliwashirikisha habari njema
watanzania kuwa inasherehekea miaka mitano tangu kuanza kufanya shughuli
zake barani Afrika kwa kuwarahisishia waafrika huduma mbalimbali kwa
njia ya mtandao.
Jumia
ambayo inaundwa na kampuni tano (Jumia Travel, Jumia Food, Jumia Market,
Jumia Deals na Classified pamoja na Jumia Jobs) pia imeujulisha umma
kuwa imefanikiwa kuingia kwenye orodha ya makampuni 50 yanayotoa huduma
za mtandaoni duniani kwa mara ya pili mfululizo.
Orodha
hiyo ilitolewa na Taasisi ya Kiteknolojia ya Massachusetts (MIT) ya
nchini Marekani ambayo huyatambua makampuni 50, yaliyopo tayari na
yanayochipukia katika kutengeneza fursa kwa kutumia teknolojia mpya
kwenye kutoa suluhu na kukidhi mahitaji ya masoko mbalimbali duniani.
Mwaka
huu 2017, Jumia imeshika nafasi ya 44 ukilinganisha na ya 47 kwa mwaka
2016, ikiwa imetajwa kama kampuni iliyojikita zaidi kutatua changamoto
zinatokana na huduma kwa njia ya mtandao barani Afrika. Changamoto hizo
ni pamoja na barabara zisizopitika kwa urahisi, tabia zisizotabirika za
wateja, kukosekana ueneaji wa kutosha wa mtandao wa intaneti ambapo
kitakwimu ueneaji wake ni asilimia 27 tu barani kote.
No comments:
Post a Comment